Ticker

6/recent/ticker-posts

JEMBE LINGINE LA ZAMBIA LILILOCHUKULIWA NA TP MAZEMBE

 IMEWEKWA OKTOBA 30,2013 SAA 9:10 ALFAJIRI
TP Mazeme katika mazoezi
Klabu ya DR Congo ya TP Mazembe imetangaza kumsaini beki wa Zambia  Chongo Kabaso kutoka Konkala Mines Polisi FC.
Beki huyo wa Kushoto mwenye umri wa miaka 21 alikuwepo 
Oktoba 15 katika mchezo wa kirafiki wa Zambia dhidi ya Brazili mjini Beijing China na alikuwa  katika kikosi cha Chipolopolo kilichoshi COSAFA Senior Challenge Cup mwezi Julai.
"Kuwasili Chongo Kabaso, nyota itapanda, ni furaha kubwa kwa upande wetu wa klaabu ya TP Mazembe," alisema Mfaransa Patrice Carteron, kocha wa nne wa mabingwa wa Caf. 
Ni dalili nyingine  nzuri ya kuwekeza katika mustakabali wa klabu na kufanya kuwa moja ya timu bora ya Afrika yenye uwezo wa kushinda  Ligi ya Mabingwa ya Caf ijayo." 

Kabaso inakuwa mchezaji wa saba wa Zambia kusaini Corbeaux baada ya Jonas Sakuwaha, Hichani Himonde, Stopilla Sunzu, Nathan Sinkala, Rainford Kalaba na Given Singuluma. Kutokana.
Mazembe watakutana na Tunisia CF Sfaxien katika fainali ya kombe la Shirikisho, Caf, mwezi ujao.
 

Post a Comment

0 Comments