IMEWEKWA OKTOBA 30,2013 SAA 7:50 USIKU
Xabi Alonso anajiandaa kucheza mchezo wake wa kwanza tangu msimu uliopita akiwa na Real Madrid katika mchezo dhidi ya
Sevilla siku ya Jumatano katika Ligi ya Hispania.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hakucheza tangu mwezi Mei kutokana na majeruhi ya mguu na kocha wa Madrid
Carlo Ancelotti anasema "Xabi yuko katika mazoezi,Na
nadhani kwamba leo atakuwa kwenye benchi letu na nitajaribu kumpa
dakika chache."
Alonso alikuwa akifanyiwa upasuaji na baada ya kupona kutoka katika operesheni alivunjika mguu wake,na hivyo kuongeza muda wa wa kuwa nje.
Alonso alikosa Kombe la Shirikisho na Hispania na wiki 10 za kwanza za msimu wa Madrid.

0 Comments