Ticker

6/recent/ticker-posts

DAVID MOYES AMPA MAKAVU LIVE WILRIED ZAHA

 IMEWEKWA OKTOBA 30,2013 SAA 7:14 USIKU


Meneja David Moyes amesema kwamba Wilfried Zaha atapewa fursa ya kuthibitisha thamani yake,na ameyasema hayo kabla ya mchezo wao wa Capital One walioibuka na ushindi wa mabao 4
kwa 0 dhidi ya Norwich City.
Zaha ambaye amejiunga na United msimu wa karibu baada ya kusaini kutoka Crystal Palace kwa ada ya thamani ya hadi £ 15 milioni, lakini kwa upande wake bado haja ng'ara sana katika Ligi Kuu yake ya kwanza.
Lakini Moyes amekubali kwamba anaweza kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 wakati wa dirisha la uhamisho Januari. 
"Sisi hatutaki kumuharakisha, Tunataka kufanya hivyo wakati sahihi.Nilivyosema napenda kuangalia (mkopo) mwezi Januari,ni kama nilitaka kuwa naye hapa kwa miezi sita kuona jinsi anavyofanya kazi na sisi." Moyes aliiambia tovuti ya United. 
  
"Nilimwambia tunataka kujaribu kuwa naye japo dakika, lakini tuna ushindani katika  maeneo mbalimbali kwetu sisi,tuna Nani, Antonio Valencia, Ashley Young, Adnan Januzaj na hata Shinji Kagawa kucheza upande wake ina maana sisi tuko imara mahali popote. 
":tunataka kumuangalia mpaka Januari, Lakini ana mengi sana katika mipango yangu na katika mawazo yangu wakati wote."

Post a Comment

0 Comments