IMEWEKWA OKTOBA 29,2013 SAA 2:14 USIKU
Mahakama ya michezo ya Shirikisho la Soka Ujerumani DFB imetoa uamuzi
kuwa mechi kati ya Hoffenheim na Bayer Leverkusen iliyozingirwa na bao
lenye utata haitarudiwa.
Mahakama hiyo imesema refa wa mechi hiyo Felix Brych
hakukiuka taratibu
za mchezo wa soka nchini Ujerumani kufuatia maamuzi yake ya kuidhinisha
bao la mchezaji Stefan Kiessling lililofungwa katika dakika ya 72 baada
ya mpira aliopiga kwa njia ya kichwa kuingia langoni kupitia nje ya wavu
katika tundu na hivyo kuipa ushindi Leverkusen dhidi ya Hoffenheim ya
mabao mawili kwa moja.
Gazeti la Westdeutsche la mjini Düsseldorf linaandika:
Kitu pekee kinachoweza kumaliza udhia ni ushahidi wa kanda ya video.
Kanda hiyo ingemuepushia zaidi Stefan Kießling lawama za kila aina. Kwa
namna hiyo, tangu yeye mpaka kufikia msimamizi wa pambano hilo
wangesalimika.
TAZAMA VIDEO YA "GOLI HEWA"

0 Comments