Ticker

6/recent/ticker-posts

STEVEN GERRARD ATOA WITO KABLA YA MCHEZO WAO DHIDI YA POLAND

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 14,2013 SAA 03:04 USIKU
Nahodha Steven Gerrard ametoa wito kwa wakuu wa juu wa timu ya Uingereza kujiandaa kwa ajili ya maamuzi ya Jumanne katika
mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Poland.
Uingereza wanahitaji pointi tatu katika uwanja wa Wembley ili kuhakikisha nafasi ya juu katika kundi H na wapinzani wao wa karibu Ukraine ambao ambao watacheza na San Marino katika mechi yao ya mwisho usiku huo huo.
Gerrard anaamini watapata kazi kubwa katika mchezo huo,lakini anaimani na wachezaji wenzeke wanaweza kuwa na subira. 
"Nadhani mbinu za Poland ni sawa na Montenegro," alisema, akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari Jumatatu kabla ya mechi yao.
"Wao wanataka kujilinda vizuri na kufanya hivyo ni vigumu,tunatakiwa na kuonyesha uvumilivu".
"Lakini kwa wachezaji kushambulia ni suala tu la wakati kabla ya kuja mafanikio,Sisi tutakuwa tunajiamini na tunataka kutumia fursa hii na tunataka kushinda".
"Wakati Roy alinipa unahodha wa kudumu baada ya Euro 2012, kazi yangu ilikuwa ni kuongoza vijana kwenda Brazil," aliongeza Steven Gerrard

Post a Comment

0 Comments