Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 15,2013 SAA 09:02 ALFAJIRI
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amerejea kujiunga na wachezaji wenzake katika mafunzo jana siku ya Jumatatu baada
ya kuendelea kupata ahueni kutokana maumivu ya paja aliyoyapata katika mechi ya La Liga dhidi ya Almeria mwishoni mwa mwezi uliopita.
Mchezaji huyo wa ghali
Duniani hakuweza kujiunga na Argentina, ambayo tayari imeshapata
nafasi ya kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil, katika mechi za mwisho dhidi ya Peru na Uruguay, ambapo yeye alibaki
Barcelona kwa matibabu.
Barca mechi yao inayofuata ya La Liga watafunga safari kuifuata Osasuna siku ya Jumamosi,
ingawa kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya AC Milan itakayopigwa Jumanne ya Oktoba 22 bado haijulikani kama kocha Gerardo Martino italeta ushindani katika mchezo huo ambao watakuwa ugenini.
"Mshambuliaji wa Barca na Argentina imechukua hatua nyingine mbele kwa kupata ahueni," walisema mabingwa hao wa Kihispania kwenye tovuti yao ya
(www.fcbarcelona.es) Jumatatu.
Messi
amefunga mabao nane katika mechi sita za La Liga msimu huu,na kufunga hat-trick dhidi ya Ajax Amsterdam katika Ligi ya Mabingwa
pekee.

0 Comments