Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 15,2013 SAA 12:02 JIONI
Rais wa timu ya Real
Madrid Florentino Perez amesisitiza tena kuwa hakuna mashaka
makubwa juu ya hali ya Gareth Bale na
anaweza kuonekana uwanjani mwishoni mwa
wiki hii.
Ripoti iliojitokeza mwishoni mwa wiki kutoka makao makuu ya Madrid lakini kwa mijibu wa gazeti la Marca ,inadai kwamba Bale alikuwa na maumivu katika mgongo wake na anaweza kuhitaji upasuaji.
Ilidaiwa kwamba mara ya kwanza kabisa wamegundua kuhusu tatizo hilo wakati Bale akifanyiwa vipimo wakati alipojiunga na timu ya Hispania katika uhamisho ambao ulivunja rekodi ya dunia
mwanzo wa Septemba.
Lakini
Perez alipuuzia madai hayo, na alikiambia kipindi cha televisheni Punto
Pelota: "Nimeshangazwa Ni vigumu kuelewa juu ya taarifa hizi za kikatili."
"Ni
mara ya kwanza mimi kusikia juu ya taarifa hizo,na gazeti pia liliandika kwamba mimi nimeambiwa kuhusu
tatizo hili wakati wa vipimo. Ni uongo kabisa."
"Mchezaji na timu yake wote tunawasiwasi kwa sababu tunamikataba na taarifa hii
inaweza kuathiri, Wameweza kuisema ana ngiri wakati yeye hana na
wanasheria wetu wanaangalia nini kifanyike."
Perez
amesisitiza Bale anaweza kuwepo katika mchezo dhidi ya Malaga na alisema:
"Gareth yuko shwari tayari na kuna matumaini ya kucheza Jumamosi".
"Yuko katika mafunzo vizuri na anataka kucheza na kuonyesha kwamba yote hii ilikuwa mwanzo mbaya na bahati mbaya."
Lakini katika hatua nyingine,meneja wa Wales Chris Coleman amesema Gareth Bale anahitaji kuchukua muda wa kukaa ili kuonyesha ubora wake katika timu ya Real Madrid.
Coleman ambaye hakumchezesha mchezaji huyo katika mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Macedonia, amesema "Nashashangazwa sana labda mpaka baada ya Krismasi ,tunaweza kumuona Gareth Bare akawa vizuri tena," alisema Coleman.
Coleman
aliongeza: "Katika kambi ya mwisho hapa, nilikuwa na mengi ya
kukosoa kwa kutocheza Bale, lakini mtu huyo, hakuwa katika mafunzo kabla ya
msimu.
Kama huna mazoezi ya kabla ya msimu na wanatarajia kuanza na kumaliza katika mchezo,lazima kutakuwa na kasoro itakayojitokeza."
"inaweza kuchukua muda kabla ya Gareth Bare kuonekana katika ubora wake,
hasa ukizingatiaziada na mazingira mapya ambayo yuko sasa."


0 Comments