Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI KUU TZ BARA:USIPITWE NA MATOKEO YA MICHEZO YOTE YA RAUNDI YA TISA OKTOBA 13

 IMEWEKWA OCTOBA 13,2013 SAA 02:13USIKU

Raundi ya tisa ya ligi kuu Tanzania bara imeendelea hii leo Jumapili (Oktoba 13 mwaka huu) kwa mechi nne katika
viwanja vinne tofauti.
Mchezo wa kwanza ulikuwa ni kati ya Ruvu Shooting na Rhino Rangers,mchezo uliopingwa katika uwanja wa Mabatini  Mlandizi,mchezo huo umemalizika kwa timu ya Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0,bao pekee la timu hiyo liliwekwa nyavuni na Elius Maguri katika dakika ya 77.
 Mgambo Shooting na Mbeya City walikipiga katika uwanja wa Mkwakwani mkoani  Tanga,mchezo uliomalizika kawa timu ya Mbeya City kuendeleza ubabe baada ya kuitandika Mgambo Shooting bao 1 kwa 0,bao pekee lililowekwa nyavuni na Jeremiah John ndani ya dakika ya 20.
Azam Fc wanarambaramba au matajiri wa bongo walikuwa wakipambana   na JKT Ruvu  katika uwanja wao wa Azam Complex jijini  Dar es Salaam,mchezo uliomalizika kwa azam Fc kuibamiza timu ya JKT Ruvu  mabao 3 kwa 0.Mabao ya Azam Fc yalifungwa na John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 12, beki Erasto Nyoni dakika ya 39 na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 90. 
Katika uwanja wa Manungu, Turiani wenyeji  Mtibwa Sugar walikuwa wakikipiga  na Oljoro JKT,mchezo uliomalizika klwa timu ya Mtibwa Sugar kuimuka na ushindi wa bao 5 kwa 2,Mabao matatu ya ya Mtibwa yalifungwa na Abdallah Juma  katika dakika ya 23, 66 na 78.Na mabao mawili yalifungwa na Juma Luizio dakika ya 5 na 31.
Na mabao ya Oljoro yamefungwa na Shaibu Nayopa dakika ya 72,na kwa mkwaju wa penalti, Amir Omar akaipatia Oljoro bao la pili katika  dakika ya 84.

Post a Comment

0 Comments