Ticker

6/recent/ticker-posts

AFRIKA:KOCHA WA BURKINA FASO ATABILI UKWELI KWA JONATHAN PITRIOPA,AWAONGEZEA MATUMAINI TIMU YAKE KUTINGA BRAZIL,LAKINI THE ELEPHANTS KWENDA NCHINI MORROCO KUTAFUTA SARE

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 13,2013 SAA 09:39 ALFAJIRI
Washindi wa pili wa taji la mataifa ya Afrika Burkina Faso wamepata ushindi wa bao  3 kwa 2  dhidi ya Algeria katika mechi
yao ya  kufuzu kombe la dunia 2014 nchini Brazil,mchezo uliopigwa mjini Ouagadougou siku ya Jumamosi.
Awali Kabla ya mchezo kocha wa Burkinafaso Paul Put alitangaza kumkosa mshambulizi wake wa kutegemewa Alain Traore ambaye alipata jeraha wakati wa michuano ya kombe la mataifa mwezi Januari na nafasi yake siku ya jana Jumamosi  ikachukuliwa na Jonathan Pitriopa ambaye kocha Put alisema anaweza kufunga mabao wakati wowote,na hatimaye ikawa kweli,kwani katika dakika ya 45 Pitriopa ndiye aliyeanza kutikisa nyavu za  Algeria kwa kuipatia bao la kwanza timu yake.
Algeria walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 50 kupitia kwa Sofiane Feghouli,kisha katika dakika ya 66 Djakaridja Kone akaipatia bukinabe bao la pili.
katika dakika ya 70 Carl Medjani akaisawazishia bao la pili Algeria na kuifanya kuwa na matumaini ya kuondoka na sare ya ugenini,lakini nyumbani ni nyumbani bwana asikwambie mtu,kwani Burkinafaso ilipata penalti katika dakika ya 86,liliyowekwa nyavuni na Aristide Bance.
Algeria ambayo imewahi kufuzu katika kombe la dunia mara tatu iliongozwa na nahodha wake Madjid Bougherra ambaye kabla ya mchezo alikiri kuwa Burkinafaso itakuwa timu ngumu kuishinda nyumbani kwao lakini wachezaji wenzake walionyesha mchezo mzuri na kuleta upinzani mkubwa kwa Burkinafaso.
Na sasa Vijana wa Stallions wana dakika 90 ugenini ili kutinga kombe la dunia nchini Brazil.

Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya timu ya Ivory Coast na Senegal,mchezo ambao umewafanya The Elephants kuhitaji sare katika mchezo wa marudiano wa kutafuta nafasi ya kushiriki kombe la dunia nchini Brazil 2014,mchezo ambao utakaopingwa nchini Morroco baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kuupiga marufuku uwanja wa Dakar kuandaa michuano ya kimataifa kwa kipindi cha mwaka mmoja,lakini katika mchezo wa jana,Ivory Coast imeibuka na ushindi wa bao 3 kwa 1.
Mabao ya Ivory Coast yaliwekwa nyavuni na Didier Drogba kwa mkwaju wa penalti dakika ya 5,kisha mchezaji wa Senegal Lamine Sané akajifunga katika dakika ya 14,na Salomon Kalou akapachika bao la tatu katika dakika ya 49.

Kwa upande wa Teranga Lions bao lao la kufuti machozi liliwekwa nyavuni na Papiss Cisse katika dakika ya 90 ambapo katika mchezo wa marudiano  timu hiyo inahitaji kushinda kwa mabao yasiyopungua 2,mchezo ambao utapigwa nchini Morroco baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kuupiga marufuku uwanja wa Dakar kuandaa michuano ya kimataifa kwa kipindi cha mwaka mmoja

Leo Jumapili, Ethiopia watamenyana na Nigeria jijini Addis Ababa, Tunisia watacheza na Cameroon jijini Tunis,  huku Ghana wakiwa nyumbani wakichuana na Misri siku ya Jumanne mjini Kumasi.
Mataifa matano ndio yatakazofuzu kuliwakilisha bara la Afrika katika michuano hiyo ya kombe la dunia nchini Brazil itakayofanyika mwezi Juni mwakani.




 

 

Post a Comment

0 Comments