IMEWEKWA OCTOBA 12,2013 SAA 08:20 USIKU
Ulikuwa ni usiku mzuri kwa vijana wa Roy Hodgson,baada ya kutoa kipigo cha nguvu kwa timu ya Montenegro katika mchezo
wao wa kundi H katika harakati za kufuzu kombe la dunia chini Brazil mwaka 2014.
Mashambulizi yalifunguliwa na Wayne Rooney,baada ya kuipatia England bao la kwanza katika dakika ya 48,kabla ya Branko Boskovic wa timu ya Montenegro kujifunga katika dakika ya 62.
![]() |
| Juu kwa juu: Wayne Rooney (No 10) akiifungia England bao la kwanza karibu kabisa na goli |
![]() |
| Bahati mbaya: Branko Boskovic (kushoto)akijifunga mwenyewe na kuiwezesha Uingereza kuongoza kwa 2-0 |
Baada ya hapo timu ya Montenegro ikacharuka na kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Dejan Damjanovic katika dakika ya 71.Bao la tatu la England liliwekwa nyavuni katika dakika ya 78 na Andros Townsend,Kisha mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge katika dakika ya 90,akaipatia timu ya England bao la nne,ila ni kwa mkwaju wa penalti uliopingwa kipindi cha lala salama.
![]() |
| Matumaini:Dejan Damjanovic (Kushoto) akiipatia bao la kufutia machozi Montenegro |
![]() |
| Zali:Andros Townsend akii fungia England bao la tatu katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa |
![]() |
| Andros Townsend alipiga bao zuri sana |
![]() |
| Andros Townsend akifurahia bao lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa |
![]() |
| Siku haikumpita: Daniel Sturridge akiipatia England bao la mwisho |
Kikosi cha England: Hart 6,
Walker 6, Cahill 6, Jagielka 7, Baines 8, Gerrard 6 (Milner 87), Lampard
6 (Carrick 65, 6), Townsend 8 (Wilshere 80), Rooney 7, Welbeck 5, Sturridge 7. Subs: Smalling, Ruddy, Gibbs, Jones, Barkley, Defoe, Lambert, Forster.
Wafungaji : Rooney 48, Boskovic 62 (alijifunga), Townsend 78, Sturridge 90 (pen).
Kadi ya njano: Walker.
Kikosi cha Montenegro: Poleksic 7, Pavicevic 4 (Beciraj 57),
Kecojevic 6, Savic 7, Jovanovic 5; Zverotic 5, Drincic 6, Boskovic 6,
Volkov 5 (Vukcevic 72, 6); Damjanovic 5, Jovetic 6 (Kazalica 81). Subs:
Blazic, Novakovic, Krkotic, Igumanovic, Janjusevic, Kasalica, Vesovic,
Dembasic.
Mfungaji: Damjanovic 71
Kadi za njano: Pavicevic, Volkov.
Refa: Alberto Undiano Mallenco (Spain)
![]() |
| Mzuka: Roy Hodgson alionnekana kuduwaa kabla ya mchezo kuanza,lakini ngoma ilivyochanganya,duu!shuhudia vituko vyake ndani ya uwanja wa Wembley |
![]() |
| Aaaa! mzee wetu huyo |
![]() |
| wacha weee! utamtaka |
First Round – Group A
First Round – Group B
First Round – Group C
First Round – Group D
First Round – Group E
First Round – Group F
First Round – Group G
First Round – Group H
First Round – Group I
World Cup Qualifying - Conmebol (INT)
|
|---|











0 Comments