Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 11,2013 SAA 08:25 USIKU
![]() |
| Mesut Ozil:Kiungo wa Arsenal na Ujerumani anfurahia maisha yake mapya jijini London |
Mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani na kiungo wa Arsenal Mesut Ozil amekubali na kueleza kuwa anapenda maisha ya Ligi kuu ya
soka nchini England.
soka nchini England.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid , ambaye alijiunga na the Gunners kwa ada ya uhamisho ya £
43million majira ya joto,kwa sasa ana wajibu wa kimataifa pamoja na wachezaji wenzake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la Dunia leo ijumaa usiku dhidi ya Jamhuri ya Ireland.
Lakini kwa sasa vyombo vingi vya habari vya Ujerumani vinaangalia juu ya maisha mapya ya Ozil jijini London.
Alisema:
"Baadhi ya watu walidhani mimi itakuwa vigumu
zaidi kuliko hivi sasa,lakini Per Mertesacker alinipa baadhi ya
'masomo ya kuishi ' na imenisaidia, hivyo siwezi kufanya vitu visivyo faa."
"London ni mji wa kuvutia kuishi na mimi nimepapenda mahali hapa katika nafasi ya muda mfupi"
"Wachezaji wenzangu wa Arsenal na wafanyakazi pamoja na makocha wote wako nyuma
yangu,wamenipa muitikio mkubwa wa kipi kikubwa ninacho waza kufanya.
Ozil akiwa ndani ya the Gunners moja ya vitu alivyofundwa ni pamoja na wimbo wa jadi mbele ya wachezaji wenzake , ingawa alikuwa ni mzoefu alikiri hakuweza kufurahia.
Akasema:
"kuimba kidogo ,kiukweli sikutaka kufanya hivyo kwa sababu sauti
yangu tu haiko juu kufanya hivyo"
Alipoulizwa
nini alichokuwa akiimba, alijibu: "ulikuwa ni wimbo wa Kituruki, kwa kuwa waaminifu,
Bila shaka, watu hawakuelewa nini nilikuwa naimba."

0 Comments