Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 11,2013 SAA 07:21 USIKU
Kijana wa Brazil Neymar ameongezeka kiwango tangu alipoondoka katika klabu ya Santos na kwenda
Barcelona mnamo
mwezi Juni na anaweza kwenda juu zaidi ya hapo na kuwa mchezaji bora
duniani, kwa mujibu wa Ronaldo Luís Nazário de Lima.
"Yeye ana nifuata mimi na nina uhakika atakuwa na kunizidi hata zaidi,"alisema mchezaji huyo wa zamani wa Brazil na
Barcelona Ronaldo akiwaambia waandishi wa habari mjini
Rio de Janeiro Alhamisi.
"Kama yeye ataendelea kuwa na ubora kama huu, atakuwa mchezaji bora duniani."
Ronaldo
alisema Neymar inaweza kurusha timu yake kwenye vizingiti vyote,wakati
ataporudi nyumbani katika nchi yake kwa ajili ya Kombe la Dunia 2014.
"Pamoja na kuwa kijana mdogo anayekosolewa,ameonyesha kiwango kizuri katika miezi
yake michache ya kwanza nchini Hispania na kwamba anaweza kun'gara
sambamba na wachezaji bora duniani kama mchezaji mwenzake wa Barca Lionel Messi na mshambuliaji wa Real
Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo"
Ronaldo, ambaye ana kampuni yake inayoshughulikia maswala ya masoko katika michezo,na pia yuko katika kamati ya maanalizi ya Kombe la Dunia, lakini kwa sasa anatumia ya zaidi ya
muda wake jijini London ambapo anasomea maswala ya biashara na masoko.

0 Comments