Ticker

6/recent/ticker-posts

UWEZO MDOGO NDIO ULIOMUONDOA NSAJIGWA:UONGOZI WA LIPULI

IMEWEKWA OCTOBA 10,2013 SAA 09:54 ALFAJIRI
Uongozi wa timu ya soka ya  Lipuli FC ya Iringa,umesema sababu pekee ya kuachana na aliyekuwa kocha wake Shadrack Nsajigwa,
ni uwezo mdogo wa kocha huyo.
Akizungumza na Jamii na Michezo Mwenyekiti wa Lipuli, Abdul Changawa ,amesema ligi daraja la kwanza ni ngumu kuliko hata ligi kuu,kwani kuna ushindani mkubwa.
"kwa mfano kila kundi unakuta timu moja inashuka mpaka ligi ya mkoa,sisi tulitakiwa kupata kocha ambaye mwenye uzoefu,lakini kwa mtu ambaye hajawai kufundisha timu,alafu unampa timu, huku kwa wakati huo huo unataka mpande daraja,kwa kweli inakuwa ni vigumu,na tilipoangalia uwezo wake tukagundua kuwa malengo yetu hayatatimia."alisema Changawa.
"wakati tunamchukua  Shadrack Nsajigwa,ni kipindi tulichokuja kuweka kambi hapo  Dar es salaam,ambapo tulicheza mechi kama 6,lakini tukiwa na Nsajigwa tulicheza mechi takribani 8,sasa mechi 8 ukiona mtu unashinda 2 una fungwa 4 na kudroo mechi nyingi,ni kigezo tosha, na hii ligi yenyewe mechi zenyewe 3,unataka kuniambia tuzidi kuendelea naye tu,ukija kushtuka ligi yenyewe imeisha,kwaiyo tumeona ni bora tuachane naye kuliko kuleta madhara mbele ya safari".aliongeza Mwenyekiti huyo wa Lipuli.

 Aidha changawa ameongeza kuwa,timu hiyo kwa sasa iko mikononi mwa kocha msaidizi,ila kama hali ya ufundishaji wa kocha huyo msaidizi itakuwa nzuri,watamchukua moja kwa moja kwa ajili ya kukinoa kikosi hiko cha Lipuli.
Pia ametoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo,kuiunga mkono timu ya Lipuli kwani ligi wanayocheza bado wana nafasi kwa mechi takribani 10,na wamepata ushindi wa kwanza kutoka kwa timu ya Maji maji ya Songea,na wana imani watafanya vizuri,ili kuziba makosa waliyoyafanya kwa mara ya kwanza,na wananchi wa Iringa wataiona Lipuli ikishiliki ligi kuu kwani kwa takribani miaka 13 hakuna timu ya Iringa inayoshiriki ligi kuu.

Post a Comment

0 Comments