Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 11,2013 SAA 09:35 ALFAJIRI
Beki wa kushoto wa Barcelona Jordi Alba atakuwa nje kwa wiki
sita baada ya kuumia mguu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 24 atakuwa katika wakati mgumu kwani inasemekana atakuwa nje kwa karibu mwezi mmoja hivi.
Barca ambayo iko juu katika msimamo wa ligi kuu baada kushinda michezo yote nane,lakini wako sawa na Atletico Madrid ila tofauti kwa mabao.
Kocha Gerardo Martino atawatumia Javier Mascherano, 29, na Carlos Puyol, 35,baada ya kurudi kutoka majeruhi.
Mascherano aliumia mguu katika mechi waliyoshinda 4-1 dhidi ya Real Sociedad, wakati nahodha wa klabu
Puyol amekuwa nje tangu March baada ya kufanyiwa operesheni kubwa ya goti .
Marc Bartra, 22, imekuwa akicheza mara kwa mara katika wiki za karibuni.
Lakini ulinzi wa wacatalan hao kuna uwezekano wa kuwa bora zaidi wakati watakapopambana na
Osasuna - baada ya mapumziko ya kimataifa, na mechi hiyo itapingwa Jumamosi ya Oktoba 19.

0 Comments