Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMA WEWE NI MFANYABIASHARA WA AINA YEYOTE,UNAYEINGIZA SHILINGI ELFU 45 KWA SIKU,TAHARIFA HII INAKUHUSU…

Na.Herman Kihwili,IMEWEKWA OCTO 3,2013 SAA 08:50 USIKU

Richard M. kayombo ni mkurugenzi wa huduma na elimu wa mamlaka ya mapato Tanzania(kushoto)
Wito umetolewa kwa wafanyabiashara wote nchini kununua mashine za risiti za  kielektroniki ,kwani ifikapo Novemba 15
mwaka huu,hakutaruhusiwa kufanya biashara pasipokuwa na mashine hizo.
Hayo yamesemwa na naibu kamishna idara ya kodi za ndani Bi.Genorose Bateyuga,na kuwataka wananchi kujua umuhimu wa kudai risiti na iwapo hawatapewa risiti wanatakiwa kutoa taharifa katika ofisi za mamlaka ya mapato nchini.
Naibu kamishna idara ya kodi za ndani Bi.Genorose Bateyuga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Aidha Genorose Bateyuga ameongeza kuwa mashine hizo zanatakiwa kutumiwa na wafanyabiashara wote wenye kuingiza zaidi ya shilingi 45,000 kwa siku,na iwapo mfanya biashara atakiuka agizo hilo,atapigwa faini ya shilingi milioni 3 na iwapo akiwa amepigwa faini lakini bado ataendelea kukiuka agizo hilo,mamlaka itachukua hatua ya kumfungia na kutangazwa kuwa uma kuwa anafanya biashara kinyume na utaratibu.
Pia Bi. Bateyuga amewataka wafanyabiashara kufika katika ofisi zao zilizozagaa kote nchini kununua mashine hizo za kielektroniki ,na kuwaomba  kuhakikisha wanaelekezwa jinsi ya kutumia mashine hizo,na kusisitiza iwapo mashine hizo zitaharibika,unatakiwa kurudisha ndani ya masaa 24 na mfanya biashara utapewa kibali maalumu cha kutumia risiti za kawaida kwa muda.
Mshine za kielektroniki ni muhimu kwa sababu zinamsaidia mteja kulipa kodi kilingana na unachokilipia.
Mamlaka ya mapato nchini Tanzania(TRA) imejipanga kikamilifu kwani tangu siku ya jumatatu ya tarehe 3 Septemba mwaka huu wafanyakazi wake wametawanyika katika sehemu mbalimbali za kupakia mizigo kama Ubungo,Temeke,Jangwani na Kisutu.

Post a Comment

0 Comments