IMEWEKWA OKTOBA 31,2013 SAA 06:24 USIKU
UEFA wamefungia sehemu moja katika uwanja wa CSKA Moscow kwa ajili ya mechi yao ya
Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich tarehe 27 Novemba kutokana na
tabia ya kibaguzi ya
mashabiki wao.
Mashabiki hao wa Urusi wameshtakiwa baada ya kutuhumiwa
kwa ubaguzi wa rangi,baada ya kukashfu kwa kuiimba wakimlenga kiungo wa Manchester City Yaya
Toure tarehe 23 Oktoba.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory
Coast alilalamika kwa refa wakati wa mchi hiyo na baada ya mechi kuhusu tuhuma hizo za
ubaguzi wa rangi lakini CSKA walikataa madai hayo wakidai hayana mashiko na ukweli.
Hata
hivyo, UEFA wameamua kuidhinisha klabu hiyo kudhibiti mashabiki wake kuwa na nidhamu,pia jopo la UEFA la kinidhamu limeamuru kufungwa kwa sehemu D ya uwanja wa Khimki katika mechi dhidi ya Bayern Munich itakayopigwa Moscow Novemba 27.
Bodi ya uongozi wamewahi kukosoa kwa ajili tu ya kutoa faini katika kesi hiyo na walisisitiza kwamba kufungwa sehemu ya misingi inawakilisha hatua
mbele katika vita dhidi ya ubaguzi.

0 Comments