Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 2,2013 SAA 07:51 USIKU
Mesut Ozil alikuwa kama akisubiri siku kama hii iweze kufika,na hatimaye ikawaidia kwani katika mchezo wa ligi ya mabingwa usiku wa jana mchezaji huyo ameweza kuwa Man of the match na pia kutupia bao moja dakika ya 8 katika mchezo huo iliopingwa katika dimba la Emirates na kushuhudia kikosi cha SSC Napoli kinachoongozwa na kocha Rafa Benitez kulala na bao 2 kwa 0.
![]() |
| Nani wa kumaliza: Ozil alitengenezewa nafasi nzuri na Aaron Ramsey ambayo ilimshinda kipa wa zamani wa Liverpool Pepe Reina aliyoko kwa mkopo Napoli |
![]() |
| Pepe Reina akikodolea macho mpira uliopigwa na Ozi, ambaye alindika bao la kwanza kwa Arsenal mapema kabisa |
![]() |
| Mimi nakujua wewe: Wenger na Rafa Benitez wakipeana mikono kabla ya kipenga kulia, lakini mechi akageuka chungu kwa bosi wa Napoli Benitez |
Mabao yote yalipatika na katika kipindi cha kwanza, na Olivier Giroud naye alitupia bao la pili katika dakika ya 15 na kuisababishia timu hiyo ya Napoli kuondoka kichwa chini.
![]() |
Oliver Giroud (katikati) akiunganisha cross ya Ozil na kuandika bao la pili kwa urahisi kabisa
|
![]() |
| Shauku: Mshabiki wa Napoli hakukata tamaa kuwahamasisha wenzake kushangilia kwenye Uwanja wa Emirates |
ANGALIA VIDEO YA MAGOLI YOTE
KIKOSI CHA ARSENAL (4-3-2-1):
Szczesny 6; Sagna 7, Mertesacker 7, Koscielny 7, Gibbs 7; Flamini 8,
Arteta 7, Ramsey 7 (Monreal 88); Ozil 9, Rosicky 6 (Wilshere 63, 6);
Giroud 7.
Akiba wasiotumoka: Fabianski, Vermaelen, Bendtner, Jenkinson, Gnabry
Kocha : Arsene Wenger
Wafungaji: Ozil 8, Giroud 15
KIKOSI CHA NAPOLI (4-2-3-1):
Reina 5; Mesto 5, Albiol 6 (Fernandez 83), Britos 6, Zuniga 5; Behrami
5, Inler 6; Callejon 5 (Zapata 77), Hamsik 6, Insigne 5; Pandev 5
(Mertens 61, 5)
Akiba: Cabral, Dzemaili, Fernandez, Armero, Cannavaro.
Kocha: Rafa Benitez
Man of the match: Ozil
Refa: Milorad Mazic (SRB) - 7
Waliohudhulia: 59,536







0 Comments