Ticker

6/recent/ticker-posts

STEAUA BUCHAREST O CHELSEA 4:ETO'O ASABABISHA BALAA,RAMIRES NI MOTO WA KUOTEA MBALI...ushahidi wa video,picha na maelezo uko hapa...

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 1,2013 SAA 06:53 USIKU
Ramires alifunga mara mbili katika mchezo wa Chelsea walioshinda 4-0 dhidi ya  Steaua Bucharest, mchezo uliokuwa wa Ligi ya
mabingwa wa Kundi E uliopigwa katika uwanja wa National Arena.
Fernando Torres akitoka nje baada ya kuumia goti na kumpisha   Samuel Eto'o katika dakika ya 11
Si siku yako: Mchezaji wa Steaua Bucharest Daniel Georgievski akiweka kiatu vizuri baada ya kujifunga bao mwenyewe
Mchezaji wa Steaua Bucharest,Danijel Georgievski alijifunga mwenyewe baada Eto'o kupiga shuti kali lililomfanya kipa kulitema na kwa bahati mbaya Danijel Georgievski akatumbukiza mpira nyavuni.
Ramires aliongoza mauaji usiku wa jana katika ushindi  kwa ajili ya Chelsea
Kutia chumvi katika majeraha: Frank Lampard (kushoto) akisherehekea baada ya kuongeza machungu kwa timu ya Steaua Bucharest  kwa kufunga bao la  4  
 Danieli Georgievski (kushoto) wa Steaua akipotezwa nje  na mchezaji wa  Chelsea  Andre Schurrle ambaye amekuwa Man of the Match
Ramires alirudi tena katika dakika ya 55 na kuizawadia timu hiyo inayoongozwa na Jose Mourinho bao la tatu,na Frank Lampard akafunga kitabu cha mabao cha timu ya Chelsea kwa kuiandikia bao la nne katika dakika ya mwisho kabisa ya mchezo huo.

ANGALIA VIDEO YA MAGOLI YOTE
KIKOSI CHA STEAUA: Tatarusanu 5; Georgievski 4 (Varela 71), Szukala 5, Gardos 5, Latovlevici 6; Bouceanu 4, Filip 5; Popa 4 (Kapetanos HT), Stanciu 4, Tanase 5; Piovaccari 5 (Tatu HT).
Wachezaji wa akiba : Nita, Prepelita, Cristea, Neagu.
Kocha : Laurentiu Reghecampf 5.
KIKOSI CHA CHELSEA: Cech 7; Ivanovic 7, Terry 6, Luiz 6, Cole 7; Ramires 8, Lampard 7; Oscar 6 (Azpilicueta 78), Mata 6 (Willian 80), Schurrle 8; Torres (Eto'o 11, 6)
Wachezaji wa akiba: Schwarzer, Mikel, Cahill, Ba.
Kadi za njano: Lampard, Cole
Kocha: Jose Mourinho 7.
Man of the Match: Andre Schurrle

Post a Comment

0 Comments