IMEWEKWA OKTOBA 23,2013 SAA 11:09 ALFAJIRI
 |
| Clash: polisi wa kutuliza ghasia wakipuliza maji ya dawa kwa mashabiki wa Napoli barabarani kabla ya mchezo |
Mashabiki wa Napoli
walikuwa katika uangalizi baada ya kukimbia ghasia kaskazini mwa London wakati wao wanakabiliwa Arsenal,
lakini hapo jana pia kulikuwa na
mapigano kati ya mashabiki na polisi wa Ufaransa na kufanya kuwe na ghasia kabla ya mechi
hii.
 |
| Katika nafasi: polisi walikuwepo ndani ya uwanja kwa ajili ya mechi |
 |
| Machoni kama watu:Mshabiki wa Napoli Wakifurahi ndani ya uwanja, kabla ya mpira kuanza ilikuwa ni mateke |
 |
| Kipigo:Shabiki Mmoja wa Napoli mbaroni kabla ya mchezo na Marseille |
 |
| Msuguano: Baadhi ya wafuasi wa Napoli wakionekana wamebeba fimbo wakikabiliana na polisi |
Lakini Katika mchezo wa jana timu ya Napoli inayoongozwa na kocha Rafa Benitez,imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Marseille katika mchezo uliopingwa nchini Ufaransa katika uwanja wa Stade Vlodrome.
 |
| Duvan Esteban Zapata akifunga bao la ushindi kwa Napoli |
 |
| Jose Callejon (katikati) akisherehekea baada ya kufunga bao la kwanza kwa Napoli |
Mabao ya Napoli yaliwekwa nyavuni na Jose Maria Callejon katika dakika ya 42 baada ya kumtoka beki na kipa wa Marseille, na bao la pili lilifungwa katika dakika ya 67 na Duvan Zapata aliyechukua nafasi ya Gonzalo Higuain dakika ya 58 .Na bao la kufutia machozi kwa upande wa Olympique de Marseille lilifungwa na André Ayew katika dakika ya 89.
Katika mchezo mwingine Neymar
na Robinho walionekana kuwa na hamu sana ya kubadilishana mashati wakati wa
mpambano wa AC Milan dhidi ya Barcelona katika Ligi ya Mabingwa usiku wa
Jumanne ... na walifanya hivyo mapema baada ya kipindi cha kwanza kuisha!
 |
| Bado mapema: Mchezaji wa AC Milan ya Robinho na Neymar wa Barcelona walibadilishana mashati kabla ya mchezo wa AC Milan v Barcelona kuisha |
 |
| Neymar alipost picha ya shujaa wake mwenyewe Robinho kwenye Instagram Jumanne |
 |
| Robinho akiongea na Neymar baada ya filimbi ya mwisho na baada ya sare ya AC Milan 1-1 na Barcelona |
Pamoja
na kuwa timu moja ya taifa, Robinho bado ni mmoja wa mashujaa wakubwa wa Neymar na ndio maana wakabadlishana mashati mapema baada ya mwamuzi kupuliza kipenga kuashilia ni mapumziko.
 |
| Robinho akiwachanganya walinzi wa Barcelona na kuweza kufunga wao la kwanza kwa Milan |
 |
| Mfungaji: Robinho akishangilia bao la kuongoza wakati wa mechi ya Kundi H Milan dhidi ya Barcelona |
Lakini katika mchezo timu hizo mbili za AC Milan na Barcelona zimechoshana nguvu kwa kutoka sare ya 1 kwa 1, na wenyeji AC Milan ndio waliotangulia kupata bao kupitia kwa Robinho mapema katika dakika ya 9.
Na bao la Barcelona lilifungwa na Lionel Messi katika dakika ya 23.
 |
| Lionel Messi akitikisa nyavu za Milan na kusawazisha kwa upande wa Barcelona |
 |
Wachezaji wa Milan, ikiwa ni pamoja na Mario Balotelli na Sulley Muntari, wakiruka wakati Messi akipiga free-kick isiyokuwa na faida.
|
0 Comments