IMEWEKWA SEPT. 24,2013 SAA 9:11USIKU

Timu ya kikapu ya Ufaransa yaandika historia kwa kutwaa kombe la ulaya
Timu ya
taifa ya kikapu nchini Ufaransa, imetwaa Kombe la mpira wa kikapo katika
mashindano ya Ulaya ikiwa ni mara ya kwanza katika Historia ya mchezo
huo.
Vijana wa Les Blues waliishinda Litunia kwa vikapo 80 kwa 66
ikiwa ni tofauti ya vikapo 14, ambapo wataalamu wa mchezo huu wanasema
ni tafauti kubwa.Wachezaji nyota waliotamba katika mchezo huo ni pamoja na Boris Diaw,
Nicolas Batum pamoja na Tony Parker alieteuliwa kuwa mchezaji bora wa
michuano hiyo ya mpira wa kikapo barani Ulaya.

Kulikuwepo na shaka upande wa Timu hiyo ya Ufransa, kwani walianza vibaya kwa kushindwa mara tatu katika mechi nane.
Lakini baadae vijana hao wa le Blues wamekamilisha kuwa washindi wa
michuano hiyo pale walipoanza kuinyuka Slovenia wenyeji wa michuano hiyo
mbele ya mashabiki wake na baadae Uhispania bingwa mtetezi wa kombe
hilo.
CHANZO:rfi Kiswahili
0 Comments