Na.Herman Kihwili.IMEWEKWA SEPT. 23,2013 SAA 3:31USIKU
Leo tarehe 23 septemba 2013 ni miaka 46 tangu madini ya Tanzanite yagunduliwe nchini Tanzania mwaka 1967,watu kadhaa nchini Tanzania wamekuwa wanajiita Tanzanite na wengine kuwapa majina watoto wao wanaozaliwa jina la Tanzanite bila kufahamu nani hasa aliyegundua madina hayo,Blog ya Jamii na Michezo imefanya mahojiano ya moja kwa moja na mgunduzi wa madini haya ya Tanzanite, Mzee Jumanne Mhero Ngoma aliyezaliwa mwaka 1939
Na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
>Kwanza kabisa Jamii na Michezo ilitaka kujua Mzee Jumanne Mhero Ngoma(Mzee Tanzanite) amefaidika vipi na madini hayo?
Mzee ngoma:Sija nufaka moja kwa moja na madini haya kwa sababu kipindi nagundua madini haya sheria ya hatimiliki haikuwepo.
>Jamii na Mchezo:Serikali ina kusaidiaje mapaka sasa?
Mzee Ngoma:siko tayari kulaumu,kwa sababu mpaka kufikia hapa ni nguvu ya Serikali.
>Jamii na Michezo:Ni kifaa kipi ulichotumia kugundua madini ya Tanzanite?
Mzee Ngoma:Nina ujuzi wa kugundua madini,sina kifaa chochote kinachoniongoza,kifa ni kichwa changu,na mpaka sasa naendelea kuchimba madini menginea ya aina ya Gipsam
![]() |
Asha Ngoma ni mwentekiti wa Tanzanite Founder Foundation akionyesha cheti cha udhibitisho wa ugunduzi wa madini ya Tanzanite kutoka serikalini |
Lakini pia Jamii na Mchezo ilitaka kujua kama anafahamu madini hayo yanatumika kwa kutengenezea kitu gani,na mzee Ngoma A.K.A mzee Tanzanite ambaye anatarajia kuwafundisha vijana njia za kutafuta masoko ya madini hayo kwa kutumia kampuni yake ya Tanzanite Founder Foundation, alisema kuwa hajui madini hayo yanatumika kwa kutengenezea kitu gani kwa sababu miaka iliyopita serikali ilitaka kumpeleka katika nchi kadhaa za ulaya ili aende akajifunze matumizi ya madini ya Tanzanite,lakini cha kushangaza alikwenda mtu mwingine kwa kutumia jina lake(ambaye hamfahamu), na yeye mzee Ngoma akaletewa Vyeti tu pamoja na Passport zilizotumika kusafiria.
0 Comments