Ticker

6/recent/ticker-posts

MESSI AMUONYA RONALDO KWA KUWEKA REKODI MPYA NA NAKUPIGA HAT-TRICK KATIKA USHINDI WA BARCELONA WA BAO 4 KWA 0 DHIDI YA AJAX

   Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 19,2013 SAA 8:00 USIKU

Lionel Messi amefanikiwa  kupiga hat-trick katika ushindi wa bao 4 kwa 0  kati ya timu yake ya Barcelona na timu ya Ajax mchezo
uliokuwa wa  Kundi H katika ligi ya mabingwa balani ulaya uliopigwa katika Uwanja wa Nou Camp.
Usahihi: Messi bao lake la kwanza lilipatikana kwa free-kick katika dakika ya 22
Mshambuliaji huyo wa Argentina alikuwa na wasaa mzuri baada ya kupiga bao lake la kwanza kwa mkwaju wa free-kick ndani ya dakika ya 22 na kisha kuzalisha bao mbili katika dakika ya 55 na 75  lakini bao la tatu la timu ya  Barcelona,alifunga Gerard Pique kwa msaada wa messi  katika dakika ya 69 kabla ya kupisha na nafasi yake kuchukuliwa na Bartra katika dakika ya  80.
Ruka juu: Pique aliiwezesha  Barcelona kwa kuipatia bao la tatu
Messi, labda  alitetemeshwa na Cristiano Ronaldo katika mchezo wa Real Madrid usiku wa Jumanne,na sasa ana mabao 62 katika michezo ya Ligi ya  Mabingwa na kuwa na rekodi ya kupiga hat-tricks 4.
Kuchanganyikiwa: Neymar alikasirika  baada ya kukosa bao,kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Pedro dakika ya  72
Kwa upande wa timu ya ajax kwa kweli walikuwa hawana bahati katika mchezo wa jana,maana walipoteza penalti iliyopigwa na Kolbeinn Sigthorsson katika dakika ya 77 na kisha penalti hiyo kupanguliwa na kipa Victor Valdes.

Kikosi cha Barcelona: Valdes, Alves, Pique (Bartra 80), Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas (Xavi 72), Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar (Pedro 72).
Akiba wasotumika :  Pinto, Montoya, Song, Tello.
Wafungaji: Messi (22, 55 & 75), Pique (69)
Kiakosi cha Ajax: Vermeer, van Rhijn, Denswil, Moisander (van der Hoorn 73), Blind (Schone 78), Poulsen, de Jong (Serero 59), Duarte, Bojan, Sigthorsson, Boilesen.
Akiba wasiotumika : Cillessen, Fischer, Sana, Hoesen. 

 BOFYA HAPA KWA MATOKEO KAMILI,RATIBA NA MSIMAMO WA LIGI YA MABINGWA BALANI ULAYA

Post a Comment

0 Comments