Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 18,2013 SAA 3:0 USIKU
Liverpool
wamethibitisha Philippe Coutinho Atakuwa nje mpaka mwishoni
mwa mwezi Oktoba baada ya kuumia bega lake katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 2-2
dhidi ya
Swansea uliopigwa siku ya Jumatatu usiku.
Mbrazil ambaye alibadilishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Iago Aspas dakika 55 kwenye Uwanja wa Liberty baada ya kuanguka kufuatia changamoto kutoka kwa nahodha wa Swansea Ashley Williams.
Mchezaji huyo mwenye Miaka
21-aliondoka uwanja huku mkono wake ukiwa umeshikilia bega na baada
ya mchezo meneja wa Liverpool Brendan Rodgers aliaelezea taharifa kuhusiana na Coutinho
"alikuwa amejeruhiwa sana tulipomuangalia katika chumba kubadilisha."
Siku
ya Jumatatu, Rodgers alisema anatumaini kuumia kwa Coutinho kulikuwa ni
zaidi ya kuvilia damu lakini sasa ni wazi kwamba kuumia kwake kulikuwa na mbaya zaidi kuliko
awali walivyofikili.
Sasa mchezaji huyo anajiunga na wenzake
Glen Johnson, Aly Cissokho na Sebastian Coates ambao wote wako nje kwa majeraha katika kikosi cha Liverpool, wakati Daniel Sturridge akirejea kikamilifu baada ya kuwa nje kwa majeraha,na kama unakumbuka alipiga bao moja katika mchezo wa siku ya jumatatu dhidi ya Swansea City.

0 Comments