Ticker

6/recent/ticker-posts

ROONEY ATIMIZA MAGOLI 200 NA UNITED,RONALDO APIGA TATU BALE AKIMUANGALIA TU,LAKINI MANCHESTER CITY NA BAYERN MUNICH WAIGANA KATIKA LIGI YA MABINGWA ULAYA

 Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 18,2013 SAA 10:08 USIKU
Wayne Rooney amefikia  historia ya kufunga mabao 200 katika klabu yake ya   Manchester United akiwa na meneja mpya David Moyes baada ya kushinda katika mchezo wao wa kwanza katika 
kampeni ya Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi.
Rooney ambaye alifunga mabao mawili katika mchezo huo ulimalio malizika kwa United kuibuka na ushindi  wa mabao 4 kwa 2 dhidi ya Bayer Leverkusen,na mchezaji huyo akafunga bao la kwanza katika dakika ya 22 kabla ya Leverkusen kusawazisha katika dakika ya 54 ya kipindi cha pili kupitia kwa Simon Rolfes.
David Moyes  ahamini kama Rooney amekosa bao

Sir Alex Ferguson kwa mbaali:

Baada ya hapo Manchester United wakazidisha mashambulizi na kuweza kupata bao la pili,bao lililowekwa nyavuni kupitia kwa Robin van Persie katika dakika ya 59,na baada ya hapo ikafuata zamu ya mzee wa kazi(Wayne Rooney)kuweka rekodi ya kufunga bao lake la 200 katika dakika ya 70.Na Luis Antonio Valencia akafunga ukurasa wa mabao  wa United kwa kuifungia bao la 4 katika dakika ya 79,lakini Leverkusen bao lao la 2 liliwekwa nyavuni na Ömer Toprak ndani ya dakika ya 88. 
Bobby Charlton
Wayne Rooney bado ajavunja rekodi ya mabao kwa timu ya Manchester United iliyowekwa na Bobby Charlton ambaye anajumla ya mabao 249 na Denis Law mwenye mabao 237 pamoja na Jack Rowley ambaye ana mabao 211.

Galatasaray Vs Real Madrid
Katika mchezo kati ya timu ya Galatasaray  na timu ya  Real Madrid,mshambuliaji wa timu ya Real Madrid , Cristiano Ronaldo ameondoka na mpira baada ya kupiga hat-trick katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya,iliomalizika kwa  timu ya Galatasaray kuambulia kichapo cha nguvu kwa kufungwa na  Real Madrid mabao 6 kwa 1.
Mabao ya Ronaldo yalipatikana katika dakika ya 63,66 na 90,mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Isco ambaye alifunga bao la kwanza dakika ya 33,na Karim Benzema akipachika mabao mawili katika dakika ya 54 na 81.
Bao la kufutia machozi la timu ya Garatasaray likifungwa na Umut Bulut dakika ya 84,huku Didier Drogba akitolewa  nje  baada ya kuumia dakika ya 46 na nafasi yake kuchukuliwa na Amrabat.

Viktoria Plzen Vs Manchester City 

Manchester City waliokuwa ugenini nao wamefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3 kwa 0 walioupata kutoka katika timu ya ktoria Plzen.
Mabao ya Man.City yote yalipatikana katika kipindi cha pili cha mchezo huo na yalifungwa na Edin Dzeko dakika ya 48,Yaya Touré dakika ya 53 na Sergio Agüero katika dakika ya 58.
Bayern Munich Vs  
CSKA Moscow
Bayern Munich amboa ni mabingwa watetezi nao wamefanya kama walivyofanya Manchester City,ila Bayern Munich wao walikuwa nyumbani na  waliwashindilia CSKA Moscow mabao 3 kwa 0.
Mabao ya Bayern Munich:David Alaba dakika ya 4,Mario Mandzukic dakika ya 41 na Arjen Robben dakika ya 68.



MICHEZO MENGINE
  Group A:



 
Real Sociedad 0 - 2 Shakhtar Donetsk
                                                 

Group B
FC København 1 - 1 Juventus
 
Group C
Benfica 2 - 0 Anderlecht

Olympiakos 1 - 4 Paris Saint Germain    
MECHI ZA LEO
Chelsea ? - ? Basel  =Stamford Bridge      
 
Schalke 04 ? - ? Steaua Bucuresti = Veltins Arena   
Marseille ? - ? Arsenal = Stade Velodrome 
SSC Napoli ? - ? Borussia Dortmund = San Paolo 
Atletico Madrid ? - ? Zenit Petersburg = Vicente Calderon
Austria Wien ? - ? FC Porto = Franz Horr Stadium
AC Milan ? - ? Celtic = San Siro
Barcelona ? - ? Ajax =  Camp Nou
  




















                 







































  

Post a Comment

0 Comments