IMEWEKWA SEPT. 28,2013 SAA 2:43 USIKU
Ligi kuu Tanzania bara imeendelea hii leo katika viwanja saba tofauti,huku macho na masikio ya wengi yakiwa katika
uwanja wa taifa katika mchezo uliomalizika kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0.
Bao pekee la Yanga ambao wamefikisha alama 9 katika msimamo, lilipachikwa nyavuni na Mganda Hamisi Kiiza katika dakika ya 63 akiunganisha kwa tik tak krosi ya Mrisho Ngassa ambaye amekamilisha adhabu yake ya kufungiwa mechi sita za mashindano na TFF pamoja na faini ya Sh. Milioni 30 na fidia ya Sh. Milioni 15, ambazo amelipa jana jumla ya Sh. Milioni 45, na hiyo ni baada ya kubainika alisaini mikataba na timu mbili za Simba na Yanga.
Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Mbeya City na timu kutoka tanga ya Coastal Union, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.Ndani ya dakika ya 7 Haruna Moshi ‘Boban’ aliipatia timu yake ya coastal union bao la kwanza,na kwa upande wa Mbeya City walipata bao katika dakika ya 70 kupitia kwa Mwagana Yeya.
Licha ya sare hiyo lakini kulitembezwa kadi nyekundu 3 katika mchezo huo kwa wachezaji Richard Peter wa Mbeya City,na Markus Ndeheli pamoja na Haruna Moshi wa Coastal ambaye alimtupia maneno machafu mwamuzi wa pembeni.
Mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani kulikuwa na mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana kati ya timu ya Mgambo Jkt na timu ya Jkt Olijoro,na katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,timu ya Kagera Sugar waliwachapa bao 1 kwa 0 timu ya Rhino Rangers, bao lililo wekwa nyavuni na Themi Felix Katika dakika ya 67.
0 Comments