Ticker

6/recent/ticker-posts

KIKAPU:MASHINDANO YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUANZA JUMAMOSI

Na.Herman Kihwili.IMEWEKWA SEPT. 26,2013 SAA 3:23 USIKU

Chama cha mpira wa kikapu kwa mkoa wa Dar es salaam ,kimeandaa mashindano ya mchezo huo kwa shule za msingi pamoja na sekondari kwa mkoa wa Dar es salaam,mashindano ya nayotarajiwa kuanza kutimua vumbi katika viwanja vya shule ya sekondali ya zanaki kuanzia siku ya jumamosi ya tarehe 28 Septemba 2013.
Makamu wa raisi wa Chama cha mpira wa kikapu kwa mkoa wa Dar es salaam Richard Jules(wa kwanza kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na kikosi cha timu ya Jkt, mara baada ya Mchezo wa fainali kati ya Oilers na JKT  kumalizika mnamo tarehe 1 Sept.2013 na timu ya Oilers iliibuka na ushindi baada ya kuichapa timu ya Jkt  kwa alama78 dhidi ya 69
 Akizungumza na Jamii na michezo Makamu wa raisi wa Chama cha mpira wa kikapu kwa mkoa wa Dar es salaam Richard Jules,amesema  mashindano hayo yatakuwa yakifanyika mara mbili
kwa wiki yaani jumamosi na jumapili na mpaka sasa maandalizi  yameshakamilika.
Shule 11 kwa upande wa wanaume na shule 4 kwa upande wanawake  zimethibitisha kushiriki,nakuongeza kuwa hizo ni shule chache,lakini bado wanatoa msisitizo kwa timu nyingine kama watajitokeza wanataka kushiriki mashindano hayo, muda bado unaruhusu.
Aidha amengeza kuwa Lengo la mashindano hayo ni kuinua vipaji katika shule za sekondari na shule za msingi,kwani vijana wengi ambao wanacheza katika ligi za mkoa wanatoka katika mashule,na vijana hao wanakuwa hawana sehemu ya uonesha vipaji vyao,na ndio maana wameamua kutumia mashindano haya ili kuweza kuibua vipaji.
"lengo kubwa ni kuangalia upatikanaji wa vijana wadogo,ambao kama chama cha mkoa tunaweza kuwatumia katika mashindano ya baadaye"alisema Richard Jules.
Lakini pia ametoa wito kwa wapenzi wa mpira wa kikapu kujitokeza kwa wingi kuangalia vijana hao,na kuwaomba wakuu wa mashule waweze kushirikana na chama ili kuweza kuruhusu shule zao ziweze kushiriki katika mashindano hayo,kwa sababu nafasi pekee wanayoweza kupata vijana hao ni kwenye umiseta tu,na sio vijana wote wanaoweza kupata nafasi ya kushiriki katika  umiseta 

Post a Comment

0 Comments