Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 3,2013 SAA 11:20 USIKU
Manchester United wamemtambulisha rasmi mchezaji wa kimataifa Ubelgiji Marouane Fellaini kutoka katika klabu ya Everton,kwa fedha inayosemekana kuwa ni £27.5million.
Marouane Fellaini mwenye umri wa miaka 25,amejiunga na
Evarton mwaka 2008,na ameshacheza mechi 163 kwa kuanza na timu ya Evarton,na mechi 10 akiwa kama mchezaji wa akiba,amefunga jumla ya mabao 32 akiwa na timu huyo.
Evarton mwaka 2008,na ameshacheza mechi 163 kwa kuanza na timu ya Evarton,na mechi 10 akiwa kama mchezaji wa akiba,amefunga jumla ya mabao 32 akiwa na timu huyo.
Boss wa Manchester United David Moyes amesema" nimefanya kazi na Marouane kwa miaka 5,na nimefurahishwa sana na uamuzi wake wa kuchagua kujiunga na Manchester
United,ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na nafikiri atareta tofauti kubwa sana katika kikosi cha United"alisema Moyes
Na kwa upande wa Marouane Fellaini amesema"nilipatwa na msisimko kusaini Manchester United,namfahamu kocha David Moyes kwa miaka mingi sasa,na naheshimu sana utendaji wake wa kazi,ikiwa nimepata nafasi ya kufanya naye tena kazi,sitaweza kuipuuzia hii nafasi,nimefanya vizuri nikiwa na Evarton na napenda kuwashukuru mashabiki wote pamoja na viongozi kwa kila kitu ambacho wamenifanyi,lakini sasa mimi ni mchezaji wa Machester United na nitafanya kila kitu kuweza kuendeleza mchango wangu katika kikosi,kwani ndio ndoto ya kila mchezaji" alisema Marouane Fellaini



0 Comments