Ticker

6/recent/ticker-posts

DANIEL STURRIDGE ANATARAJIWA KURUDI KATIKA KIKOSI CHA LIVERPOOL

Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 13,2013 SAA 4:19 USIKU
Brendan Rodgers amesema Daniel Sturridge  anaweza kuwa vizuri katika mchezo wa  Ligi Kuu dhidi ya  Swansea City siku ya
Jumatatu licha ya mshambuliaji huyo kukosa michezo miwili ya kufuzu kombe la  Dunia na timu yake ya taifa la  England kwa sababu ya kuumia.
Sturridge , ambaye amefunga mabao matano kwa Liverpool , ikiwa ni pamoja na kushindi katika michezo yote mitatu ligi kuu,na na Rodgers anamatumaini atarudi kuendelea kusaidia timu hiyo.
Baada ya kupata majeraha katika mguu na kumzuia kucheza katika michezo ya  nchi yake dhidi ya Moldova na Ukraine na kusababisha maneno maneno katika magazeti, lakini Rodgers alisema dhamira  ya Sturridge nchini Uingereza haipaswi kuhoji. 
"walikuwa ni wataalam wa tiba ambao walifanya uamuzi - na si Daniel Sturridge,Amerudi,kwani kulikuwa na maboresho kidogo," Rodgers aliwaambia waandishi wa habari. 
Liverpool  wanaoendesha wimbi la matumaini, hasa baada ya kummchapa Manchester United kabla ya mapumziko ya kimataifa, na kikosi cha Rodgers kimeonekana kuimarika baada ya kupatikana kwa nyuso tatu mpya ambazo zinatarajiwa kuwepo katika mchezo dhidi ya Swansea.
Walinzi Tiago Ilori na Mamadou Sakho walikuwa wamesaini siku ya tarehe ya mwisho ya dirisha la usajili kufungwa kama ilivyokuwa mchezaji wa Chelsea  Victor Muses aliyechukuliwa kwa mkopo wa muda mrefu na wote wanaweza  kuwa sehemu ya wachezaji watakao cheza siku ya  Jumatatu. 
 

Post a Comment

0 Comments