AC Milan huenda
ikawasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Delle Ali 25, kwa
mkopo. (Gazzetta dello Sport)
Kipa wa Manchester United na England Dean Henderson, 24, anatarajiwa kutia saini ya mkopo katika klabu ya Newcastle siku ya misho katika dirisha la uhamisho. (Talksport)
Mshambuliaji
wa Barcelona Ousmane Dembele, 24, huenda akaondoka katika klabu hiyo ya
Uhispania na licha ya kuweka makubaliano na PSG , Manchester United imeingia
katika kinyan5'ganyiro cha kumsaini mshambuliaji huyo wa Ufaransa kwa dau la
€20m (£16.6m). (Journalist Pedro Almeida)
Tottenham
pia ina hamu ya kumsaini Dembele , lakini haiko tayari kulipa mshahara
anaotaka. (Marca)
Mshambuliaji
wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32, amekubali kuendelea kucheza
katika klabu hiyo ili kumaliza kipindi cha msimu uliosalia na klabu ya
Barcelona , lakini anahitaji klabu hiyo ya Uhispania kumuuza Dembele mwanzo .
(Sport)
Ombi la
pili la Crystal Palace la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Eddie
Nketiah limekataliwa , licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa
England kusalia na kandarasi ya miezi sita pekee . (Sky Sports)
Hatua ya
Lyon ya kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele kwa mkopo
imepiga hatua , lakini mkwamo mkubwa katika majadiliano hayo ni hatua ya kutaka
kumnunua mchezaji huyomwenye umri wa miaka 25.
Chelsea
imewasilisha ombi la kutaka kumsaini winga wa Leeds na Brazil Raphinha , lakini
huenda mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atapatikana katika dirisha la
uhamisho la msimu wa joto. (Daily Mail).
Vvvvv
Beki wa
Liverpool na Wakes Neco Williams , 20, huenda akauzwa kwa mkopo huku klabu ya
Bournemouth ikiwa na hamu naye. (Liverpool Echo)
Kiungo wakati wa Mali Brighton Yves Bissouma,
25, huenda akaondoka huku Aston Villa , Tottenham na Manchester United wakiwa
nah amu ya kumsajili (Journalist
Liverpool walifanya usajili mkubwa zaidi katika dirisha hili nchini Uingereza siku ya jana Jumapili, kwa winga wa Porto kutoka Colombia Luis Diaz akijiunga kwa mkataba wenye thamani ya euro 45m (£37.5m), na euro 15m zaidi (£12.5m) kama bonasi zinazowezekana.
Newcastle tayari wamemnasa kiungo wa Lyon Mbrazil Bruno Guimaraes kwa £35m na nyongeza za £6.6m, mshambuliaji wa Burnley Chris Wood kwa £25m na beki wa kulia wa Atletico Madrid na Uingereza Kieran Trippier kwa £12m.
Kumekuwa na wachezaji wengine wanne waliosajiliwa kwenye Premier League wenye thamani ya £10m au zaidi.
Aston Villa ilimsajili beki wa kushoto wa Everton Lucas Digne kwa £25m, huku Everton ilinunua mabeki wawili kwa jumla ya £27m - Nathan Patterson wa Rangers na Vitalii Mykolenko wa Dynamo Kyiv.
Wolves walifanya usajili wa mkopo wa fowadi wa RB Leipzig Hwang Hee-chan kuwa wa kudumu kwa pauni milioni 14.
Usajili mkubwa zaidi barani Ulaya ulikuja wakati Juventus ilipomsajili fowadi wa Fiorentina Dusan Vlahovic - ambaye alikuwa akilengwa na timu kadhaa za Ligi Kuu - kwa pauni milioni 58 za awali.
Aston Villa, Brentford na Southampton zote zilisajili makipa kwa mkopo au kama wachezaji huru, huku Watford wakileta wachezaji watano ambao hawakujulikana kiasi - Edo Kayembe, Samir, Hassane Kamara, Maduka Okoye na Samuel Kalu.
Villa pia ilimsajili mlinzi wa Arsenal Calum Chambers kwa uhamisho huru.
Dili kubwa za mkopo zilipelekea Villa kumchukua Philippe Coutinho wa Barcelona na kumpeleka Anwar El Ghazi Everton, huku Wolves wakimsajili winga wa Ureno Chiquinho kutoka Estoril kwa £3m.
Wachezaji wawili waliotakiwa kuondoka kwenye Ligi ya Premia kwenda La Liga kwa mkopo walikuwa Adama Traore (Wolves kwenda Barcelona) na Anthony Martial (Manchester United kwenda Sevilla), huku United walimtoa kwa mkopo Amad.
0 Comments