Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA 08,SEPT.2018 SAA 10:22 USIKU
..>>.....
John Steven Akhwari ni mwanariadha mstaafu. Alizaliwa mwaka 1938 kule
Mbulu- Mkoani Manyara.
Aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
Olimpic mwaka
1968 nchini Mexico, katika mashindano ya riadha ya
kilomita 42. Washiriki walikuwa 75, lakini waliomaliza shindano ni 57
pekee, huku John Steven Akhwari akimaliza wa mwisho kabisa.
Baada ya mbio kuanza, walipofika kilomita ya 19, mshiriki mojawapo
alimparamia, kumsukuma na kuanguka vibaya mno. Aliumia begani, na goti
la mguu wa kulia lilitenguka.
Gari la huduma ya kwanza lilimfikia na
kumpa matibabu, akaweza kusimama tena na kuendelea na riadha.
Mwishoni kabisa, waandishi wa habari walimuuliza, Kwa nini aliendela
kukimbia ili hali ameumia kiasi hicho? Aliwaambia Nchi yangu Tanzania
haikunituma maili 5000 kuja Mexico kuanza hili shindano bali walinituma
kumaliza shindano.
Amezungumza na Herman Kihwili na kwanza anaelezea safari yake ya hivi
karibuni ambapo ametoka nchini Mexico baada ya kupata mualiko maalum.
BOFYA CHINI KUSIKILIZA
0 Comments