Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 30,2018 SAA 02:00 USIKU
,..
Mwenyekiti wa CHABADA Hussein Ally |
Wakati zoezi la uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo wa Baiskeli Tanzania (CHABATA) likianza jana Agosti 30 chini ya usimamizi wa Baraza La Michezo Taifa (BMT) uongozi wa chama cha mchezo huo mkoa wa Dar es salaam (CHABADA) nao umethibitisha kuwa katika hatua ya mwisho kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Septemba 09.
Mwenyekiti wa CHABADA Hussein Ally amezungumza na kipindi hiki na kusema kuwa, taratibu zote za kuelekea kwenye uchuguzi mkuu zinakwensa vizuri na wana imani wadau wote wa mkoa wa Dar es salaam watashiriki kikamilifu.
Katika hatua nyingine Hussein Ally amesema baada ya uchaguzi mkuu wa CHABADA, kutakua na michuano ya mbio za Baiskeli mkoa ambayo itafanyika kabla ya kuanza kwa zoezi la uchaguzi mkuu.
Wakati huo huo kiongozi huyo wa CHABADA akaendelea kutoa maelezo kuhusu michuano ya Baiskeli mkoa wa Dar es salaam septemba 09.
BOFYA CHINI KUSIKILIZA
,..
0 Comments