Klabu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi
ya klabu ya Al Masry kutoka nchini Misri siku
ya Jumatano ya tarehe 7/3/2018
katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.ya Jumatano ya tarehe 7/3/2018
![]() |
| Msemaji wa Simba Sc Haji Manara Akizungumza hii leo na waandishi wa habari(Hawapo Pichani) |
I.
VIP A – Tsh 20000
II.
VIP B - Tsh 15000
III.
Mzunguko/Orange – Tsh 5000.
Tiketi za kuingilia uwanjani siku hiyo zitaanza kuuzwa siku ya Jumatatu kwa
mawakala wa Selcom na vituo vitakavyotangazwa hapo baadae.
Klabu inawaomba mashabiki na wapenzi wa klabu kujitokeza kwa wingi siku
hiyo kuishangilia timu yao itakapokuwa inacheza, aidha inawakumbusha kununua
tiketi za mechi hiyo kwa wakati.
Katika hatua nyingine,Klabu ya Al Masri
inataraji kuwasili nchini siku ya Kesho Jumapili majira ya saa 12
jioni,na itafanya mazoezi siku ya Jumatatu jioni katika Uwanja Taifa.
Pia,waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Afrika kusini wanatarji kuwasili
nchini siku ya Jumatatu saa 10 jioni.

0 Comments