Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 05.2016 SAA 11:00 JIONI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za kifo cha kushtukiza cha Mchezaji
Ismail Halfan wa
timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza
kilichotokea Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani
Kagera.
Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu
ya Vodacom, ilikuwa Kituo cha Bukoba katika Ligi ya vijana ambayo kwa
msimu huu imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa
kituo cha Dar es Salaam.
Ismail aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza
uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa
za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.
Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha
mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua
hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake
umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa Kagera.
Inna Lillah wainna ilayhi Rajiuun. Mwenyezi Mungu, Subb Hanna Watallah ampumzishe mahali pema peponi roho ya marehemu huyu.
0 Comments