Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 08.2016 SAA 01:10 USIKU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (TFF), Bw. Issa Hayatou
ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania
(TFF), Bw. Jamal Emil Malinzi kutokana na kifo cha ghafla cha Mchezaji
Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20
wa Mbao FC ya Mwanza.
“Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mchezaji Ismail
Mrisho Khalfan akiwa na umri mdogo wa miaka 19 baada ya kuzimia katika
mchezo wa Ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20,” ilisema
sehemu ya barua hiyo ya Rais Hayatou kwenda kwa Rais Malinzi.
“Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF, familia nzima ya mpira wa
Afrika na kwa niaba ya jina langu binafsi, tunapenda kupeleka rambirambi
zetu kwa familia ya marehemu na familia ya mpira wa miguu katika
Tanzania kwa ujumla wake kufuatia kifo hiki ambacho hakikutarajiwa,”
ilisisitiza.
Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini
ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza, kilitokea Desemba 4, 2016 kwenye
Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera wakati timu yake ikicheza mchezo
huo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu
ya Vodacom, ilikuwa Kituo cha Bukoba katika Ligi ya vijana ambayo kwa
msimu huu imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa
kituo cha Dar es Salaam.
Ismail aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza
uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa
za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.
Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha
mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua
hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake
umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa Kagera. Marehemu Ismail Mrisho
Khalfan alizikwa Desemba 5, 2016 jijini Mwanza.
0 Comments