Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 08.2016 SAA 01:10 USIKU
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer),
kesho Ijumaa Novemba 9, 2016 inatarajiwa kucheza na
Uganda katika mchezo
wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Viwanja vya Karume, Ilala jijini
Dar es Salaam.
Mchezo huo ni maandalizi kwa timu Tanzania na Uganda kujiandaa na
michuano ijayo ya kimataifa ndani ya bara la Afrika na ile la CAF. TFF
inatangaza kuwa mchezo huo hautakuwa na kiingilio.
Waamuzi wa mchezo huo watakuwa Jackson Msilombo, Kessy Ngao, Heri Sassii na mtunza muda anatarajiwa kuwa Idd Maganga.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Beach Soccer, John Mwansasu anatambia nyota wake 12 wakiwamo makipa Rajab Galla na Khalifa Mgaya.
Mabeki ni Roland Revocatus, Juma Ibrahim, Kashiru Salum na Mohammed
Rajab wakati Viungo ni Mwalimu Akida, Ahmada Ali na Samwel John huku
washambuliaji wengine wakiwa ni Kassim Kilungo na Talib Ally pamoja na
Ally Rabbi ambaye ni Nahodha na Mshambulaji wa timu hiyo.
Hivi karibuni kikosi hiki kilicheza na Ivory Coast katika michezo
miwili ya kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa yAfrika
kwa soka la ufukweni bila mafanikio.
0 Comments