Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.NOV 19.2016 SAA 09:24 ALASIRI
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja
wa wachezaji wa
Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana
wenye umri wa chini ya miaka 17, mwaka huu lilimkatia rufaa mchezaji
Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, Langa Lesse
Bercy, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko
Cairo, Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo
cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).
TFF iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia
gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake pamoja na kulipia
gharama za vipimo. TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.
Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini
Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari
wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili kuwa shuhuda wa
zoezi la kipimo hicho.
Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji
Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo
lililoko "vitani",eneo hilo halikutajwa.
TFF inaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .
0 Comments