Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.NOV 25.2016 SAA 11:29 JIONI
Uongozi wa klabu bingwa Tanzania bara Young
Africans, hatimae hii leo umemtambulisha Kocha George Lwandamina kuwa mkuu wa
benchi la ufundi la klabu hiyo badala ya Hans van der Pluijm.
Makamu mwenyekiti wa Young Africans Clement Sanga alikamilisha
jukumu la kumtambulisha kocha huyo kutoka nchini Zambia mbele ya waandishi wa
habari.
Sanga amesema wakati Lwandamina anakabidhiwa
jahazi la kuongoza benchi la ufundi, aliyekua kocha mkuu klabu hapo Hans van
der Pluijm amepanda cheo na kuwa mkurugenzi wa ufundi.
Kwa upande wa George Lwandamina amesema atapambana vilivyo
kuhakikisha anafanya vema huku akikiri kuwa na jukumu zito la kutetea ubingwa
wa Tanzania bara.
Amesema anaamini wachezaji watatoa ushirikiano
dhidi yake licha ya matarajio ya utambulishi mpya wa mfumo ambao anatarajia
kuutumia kwa ajili ya kuongeza chachu ya ushindani katika kikosi pamoja na kwa
timu pinzani.
Mbali na wachezaji ambao watakua karibu na kocha
huyo, Lwandamina pia ameomba Wanayanga kumpa ushirikiano ili kufikia malengo yanayokusudiwa.
0 Comments