Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.28,2016 SAA 10:45 JIONI
Uzinduzi wa Ligi ya Taifa ya Wanawake unatarajiwa
kufanyika Novemba 1, 2016 kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
katika
mchezo ambao Baobao itacheza na Victoria Queens ya Kagera.
Ligi hiyo ya kwanza kufanyika nchini Tanzania, lakini pia kwa nchi za
Afrika Mashariki na Kati imetokea kuvutia wadau kadhaa wakiwamo Azam Tv
ambao wamedhamini kwa kuonyesha mubashari (live), michezo hiyo 30
itakayofanyika viwanja mbalimbali.
TFF imepeleka uzinduzi huo Dodoma ikiwa na lengo la kuhamasisha soka
mikoani tofauti na Dar es Salaam ambako ilizoeleka zaidi miaka ya nyuma
kabla ya kuwa na mpango wa mashindano ya aina hiyo yanayoshirikisha timu
12 kutoka kona mbalimbali za nchi.
Kadhalika, kwa siku ya Novemba mosi ya uzinduzi huo vingozi wengi wa
Serikali wakiwamo wabunge wanatajiwa kuwa Dodoma ambako watapata fursa
pekee ya kushuhudia burudani ya mpira wa miguu wa ushindani
itakayosukuma hamasa ya kutoa michango yao mbalimbali kwa ajili ya soka
la wanawake.
Mbali ya mchezo huo wa kundi B kati ya Baobao na Victoria, michezo
mingine itakuwa ni kati ya Sisterz na Panama utakaofanyika Uwanja wa
Tanganyika huko Kigoma wakati Marsh Academy ya Mwanza itacheza na
Majengo Women ya Singida kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kundi A kutakuwa na michezo mitatu ambako Viva Queens ya Mtwara
itacheza na Mburahati Queens ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Nangwanda
Sijaona wakati Fair Play ya Tanga itapambana na Evergreen ya Dar Salaam
katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga huku JKT
Queens ikiwa ni wenyeji wa Mlandizi Queens ya Pwani kwenye Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.
0 Comments