Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 11,2016 SAA 02:51 USIKU
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshuka kwa nafasi moja kutoka 123 mpaka nafasi ya 124 Katika viwango vipya
vya Shirikisho la soka duniani (FIFA) vilivyotangazwa hii leo Agosti 11 ambapo ni orodha mpya ya viwango vya kila mwezi kwa timu za mataifa yote duniani.
vya Shirikisho la soka duniani (FIFA) vilivyotangazwa hii leo Agosti 11 ambapo ni orodha mpya ya viwango vya kila mwezi kwa timu za mataifa yote duniani.
Tanzania imefanikiwa kupata pointi 300 ikishika nafasi ya tano kwa nchi za Afrika Mashariki ikiongozwa na Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.
Kwa dunia Argentina imeendelea kuongoza kwenye chati hizo.
Timu ya Argentina inaendelea kushika namba moja kama timu bora zaidi duniani huku ikiwa na pointi 1585 ikifuatiwa na Ubelgiji (1401), Colombia (1331), Ujerumani (1319) na nafasi ya tano imechukuliwa na Chile yenye pointi 1316.
Aidha viwango hivyo vimeonyesha kuwa kwa Afrika timu ya taifa ya Algeria ndiyo inaongoza ikiwa nafasi ya 32 huku ikiwa na pointi 781 ikifuatiwa na Ghana, Ivory Coast na Senegal ikishika nafasi ya nne.


0 Comments