Ticker

6/recent/ticker-posts

MECHI YA AZAM FC NA AFRICAN LYON KUPIGWA USIKU,ALASIRI KUNA WA SAUZI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 18,2016 SAA 10:38 JIONI
Azam FC  imeanza kwa vema msimu huu kwa kutwaa taji hilo kama ilivyofanya msimu uliopita kwa kubeba Kombe la
Kagame, inatarajia kuanza safari yake ya kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzani Bara (VPL) keshokutwa Jumamosi kwa kumenyana na African Lyon.
Mchezo huo unaotarajia kuwa mkali na wa aina yake utafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, ambapo awali ulitakiwa upigwe saa 10.00 jioni, lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limebadili muda na kuupeleka hadi saa 1.00 usiku.
TFF imebadilisha muda huo, ili kuiwezesha timu ya Taifa ya vijana ya Afrika Kusini (U-17) ‘Amajimbos’ kuweza kuutumia uwanja huo saa 9. 00 Alasiri siku hiyo kufanya mazoezi yake kama sheria za Shirkisho la Soka Afrika (CAF) zinavyotaka kabla ya kurudiana na vijana wa Tanzania ‘Serengeti Boys Jumapili ijayo.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments