Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kutoa
tahadhali kwa timu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL) juu
ya kuwatumia wachezaji ambao imewasajili, lakini imebainika mbele ya
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwamba wanamatatizo kwenye
usajili wao.
Majimaji ya Songea
Mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole
ambaye pia amebainika kuwa ndiye Gerald Mpole wa Majimaji ya Songea
amefungiwa kucheza soka kwa mwaka kwa kosa la kubadili jina akiwa na
lengo la kufanya udanganyifu kwenye usajili. Majimaji imeagizwa
kutomtumia mchezaji huyo kutoka Kimondo FC.
Mwadui FC ya Shinyanga
Mchezaji William Lucian aliyesajiliwa na Mwadui ya
Shinyanga kutoka Ndanda ya Mtwara, naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa
la kusajili Mwadui FC ilihali akiwa hajamaliza mkataba na Ndanda.
Mwadui isimtumie mchezaji huyo.
Mbeya City ya Mbeya
Mchezaji Saidi Mkopi, pia amefungiwa mwaka mmoja
kwa kosa la kujisali timu mbili. Imebainika kuwa akiwa bado na mkataba
na Tanzania Prisons ya Mbeya hivyo Mbeya City isi1mtumie mchezaji huyo.
African Lyon ya Dar es Salaam
Mchezaji Rehani Kibingu aliyesajiliwa na African
Lyon ya Dar es Salaam, amesimamishwa kuchezea timu hiyo mpaka uongozi wa
African Lyon kumalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam kabla ya
Agosti 27, 2016. African Lyon isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.
Mbao FC ya Mwanza
Mchezaji
Emmanuel Kichiba aliyesajiliwa Mbao FC, naye amesimamishwa mpaka Mbao
watakapomalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam, kabla ya Agosti 27,
2016. Mbao FC isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.

0 Comments