Ticker

6/recent/ticker-posts

KOCHA WA MAKIPA AZAM FC ATOA TOFAUTI YA MAKIPA WA TANZANIA NA HISPANIA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY 14,2016 SAA 08:49 MCHANA
KOCHA Mkuu wa makipa wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Jose Garcia, amesema kuwa
makipa aliowakuta ndani ya timu hiyo wapo vizuri.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz hivi karibuni, Jose alisema kuwa jambo kubwa wanalokosa ni mbinu, hivyo amejipanga kulifanyia kazi suala hilo.

“Azam ni timu nzuri na ina uwezo mkubwa sana, kiwango cha makipa niliowakuta kipo vizuri, cha muhimu ni kujituma zaidi na kuzidisha mbinu ili wawe bora zaidi kwa baadaye,” alisema.

Tanzania vs Hispania

Kocha huyo hakusita kuelezea utofauti wa makipa kutoka Tanzania na Hispania mara baada ya kuwaona wa Azam FC, ambapo alisema magolikipa wa hapa wana nguvu sana lakini wanakosa mbinu.
“Watanzania wana nguvu sana, ila wanakosa mbinu, lakini kwa upande wa kule Hispania wako vizuri zaidi na wanazo mbinu, na hicho ambacho nimeongea na wenzangu ili tuweze kukifanyia kazi,” alimalizia kocha huyo mwenye umbile kubwa na mrefu atayesaidiana majukumu hayo na Idd Abubakar.
Ukiondoa makipa wa Azam FC, Aishi Manula, Mwadini Ally na Metacha Mnata aliyepandishwa kutoka timu ya vijana na Kauju Agustino wa Azam B wanaendelea kufanya maandalizi ya msimu mpya, kuna makipa wengine wawili wa kigeni wanawania nafasi moja ya kusajiliwa, Daniel Yeboah (Ivory Coast) na Juan Jesus Gonzalez (Hispania).
Mabingwa hao wanaingia tena sokoni kutafuta golikipa mara baada ya kuachana na kipa mkongwe Ivo Mapunda, aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo msimu uliopita, ambapo anasajiliwa mwingine kuziba nafasi yake ili kuimarisha zaidi kikosi na kuleta ushindani zaidi kwenye nafasi hiyo.


Azam FC yampokea straika wa Ivory Coast


Katika hatua nyingine mshambuliaji Ibrahima Fofana kutoka nchini Ivory Coast ametua nchini siku ya Jumanne mchana tayari kabisa kufanya majaribio ya kujiunga na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC.

Mabingwa hao kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kukifanyia marekebisho kikosi chake na moja ya eneo walilolimulika ni kuboresha eneo la ushambuliaji kwa kusajili washambuliaji wapya wawili wenye viwango vya juu.

Fofana (26), ametua nchini akitokea timu ya Union Sportive de Ben Guerdane ya Tunisia aliyokuwa akiichezea msimu uliopita uliomalizika Juni 14 mwaka huu.

Nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza namba 9, 7 na 11, kabla ya kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Tunisia (Ligue 1) alikuwa akikipiga kwa miamba ya Ivory Coast Asec Mimosas tokea mwaka 2013 hadi 2015.

Akizungumza na mtandao wa www.azamfc.co.tz mara baada ya kutua, Fofana alisema nia yake kubwa ni kuisaidia Azam FC kwenda kimataifa zaidi endapo atafuzu majaribio hayo.

“Ninafuraha kabisa kukaribishwa na Azam FC, ni furaha yangu kuwepo hapa  na nimekuja kuonyesha kipaji changu lakini pia kuisaidia timu kwenda kimataifa zaidi katika michuano mikubwa ya kimataifa, kwa hiyo nadhani timu wataweza kushuhudia kipaji changu na ni Mungu pekee ndiye ataisaidia nipite salama,” alisema.

Fofana ataanza rasmi majaribio yake keshokutwa Ijumaa kikosi cha Azam FC kitakapoendelea na mazoezi yake, ambapo kesho Alhamisi ni siku ya mapumziko.

Mshambuliaji huyo anaungana na makipa wawili wa kigeni, Daniel Yeboah (Ivory Coast) na Juan Jesus Gonzalez (Hispania), wanaoendelea kufanya majaribio ndani ya Azam FC wakigombea nafasi moja ya usajili ya golikipa.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments