Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKAZI WA MBEYA KUISHUHUDIA MBEYA CITY VS YANGA KWA KIINGILIO HIKI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.9,2016 SAA 01:09 USIKU

Maandalizi ya mchezo namba 218 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya Mbeya City fc na Yanga ya Dar es
Salaam uliopagwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa yamekamilika na kinachosubiriwa ni dakika 90 hapo kesho.

Kwa mujibu wa msimamizi wa kituo cha Mbeya ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha soka mkoa, Haroub Suleiman, mchezo huo utafanyika kama ulivyopangwa kwa sababu timu zote mbili tayari zisharipoti (kuwepo) kituoni na tayari makubaliano juu ya kiingilia yashafikiwa.

“Yanga wamewasili asubuhi ya leo, hii ina maana kuwa mchezo upo kama ulivyopangwa, kutokana na uzito wa mchezo wenyewe,tumekubaliana kiingilio kitakuwa shilingi 5000, nawaomba mashabiki wote wa soka katika kanda hii ya nyanda za juu kusini wajitokeze kwa wingi kuzishangilia timu zao huku pia wakitakiwa kudumisha amani kabla na baada ya mchezo” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mbeya City Fc, Mussa Mapunda amewatakia kila la kheri na kuwashukuru mashabiki wote wa timu yake popote walipo ndani na nje ya nchi kwa jinsi walivyojitolea kuisapoti timu yao tangu ilipopanda daraja na kuwataka kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuja kuisapoti na kushuhudia City ikiandikisha ushindi wa kwanza mbeya ya Yanga.

“Pambano hili nalifananisha na lile la ki’ Biblia linalowahusu Daud na Goliatti, kwa kila hali tumepania ili tuibuke na ushindi, lakini ushindi wetu utaletwa pia na mshikamano kutoka pande zote tatu kwa maana ya uongozi, wachezaji na mashabiki, tumeiandaa timu vizuri na najua mashabiki wetu wako tayari muda wote,naomba wajitokeze kwa wingi waje na mashamsham ya kila namna ili kuhakikisha tunashinda mchezo huo, Nyumbani kwanza, Objective to win” alisema.


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .


Post a Comment

0 Comments