Ticker

6/recent/ticker-posts

UAMUZI WA RUFAA YA KIPA WA SIMBA NA GEITA GOLD KUTOLEWA KESHO

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.2,2016 SAA 11:35 JIONI
Denis Richard Dioniz,kipa wa klabu ya simba aliyeko kwa mkopo katika klabu ya Geita Gold
Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kesho Jumanne Mei 3, 2016 saa 5:00 asubuhi
itatangaza uamuzi wa rufaa nane zilizowasilishwa na kujadiliwa za viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara 2015/2016.
 Kamati hiyo itatangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Jumla ya rufaa nane zinazohusu timu, kocha, viongozi na mchezaji mmoja zilijadilikuwa na kamati hiyo kwa Jumapili Mei mosi, 2016 kwenye ofisi za TFF jijini.
Rufaa zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni za:
1.   Timu ya Geita Gold
2.   Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
3.   Denis Richard Dioniz - Kipa wa Geita Gold
4.   Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
5.   Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
6.   Timu ya Soka ya Polisi Tabora
7.   JKT Oljoro Fc ya Arusha
8.   Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
Wadau hao wa soka walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza. Wakata rufaa wote walihudhuria kikao cha rufaa zao.    

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments