YANGA SC wamefanikiwa kutwaa taji lake la pili la nyumbani katika msimu wa 2015/2016, baada ya kuifunga
Azam FC mabao 3-1 na kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) siku ya Jumatano May 25,2016 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Azam FC mabao 3-1 na kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) siku ya Jumatano May 25,2016 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Bao bao la kwanza la Yanga la Yanga lilifungwa na mshambuliaji kutoka Burundi, Amissi Tambwe dakika ya tisa ya mchezo kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.
Dakika ya pili tu baada ya kuanza kipindi cha pili, Tambwe tena akawafungia Yanga bao la pili, akimalizia krosi ya winga Simon Msuva.
Mshambuliaji Didier Kavumbangu akaifunga timu yake ya zamani, Yanga SC dakika ya 48 kwa kifua kumalizia krosi ya winga Ramadhani Singano ‘Messi’.
Kiungo Deus Kaseke akaifungia Yanga bao la tatu dakika ya 81 kwa shuti kali akimchambua kipa Aishi Manula baada ya kupata pasi ya Msuva.
ANGALIA PICHA
![]() |
Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul ameibuka mchezaji bora wa kombe la FA (Azam Sports Federation Cup)
|
![]() |
| Golikipa wa Azam FC Aishi Manula ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mashindano ya FA |
![]() |
| Atupele Green akiwa amenyanyua juu tuzo yake ya ufungaji bora akiwa amefanikiwa kufunga magoli matano kwenye michuano ya F |












0 Comments