Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMUSOKO NA NGOMA KUIKOSA MECHI YA YANGA NA ESPERANCA,VIINGILIO HIVI HAPA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.7,2016 SAA 01:40 USIKU
Uongozi wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi yote muhimu ya mchezo dhidi ya GD Sagrada
Esperanca ya Angola wa kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.
Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa Jukwaa la VIP “A” kuwa ni Sh 30,000; VIP “B” na “C” Sh 20,000 wakati jukwaa la viti Rangi ya chungwa ni Sh 7,000 wakati mzunguko wa viti vya bluu na kijani ni Sh 5,000.
Kwa mujibu wa Muro, Yanga itawakosa wachezaji mahiri wawili, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko ambao watatumia mchezo huo kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano walizoonywa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kushuka kucheza Kombe la Shirikisho.
“Tunawaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga tujitokeze kwa wingi kesho kuishangilia timu yetu kwa nguvu na kasi kubwa,” amesema Muro ambaye alitumia nafasi hiyo kutamba kwamba Yanga ilisajili wachezaji 24 kwenye michuano inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .


Post a Comment

0 Comments