Ticker

6/recent/ticker-posts

HAYA NI MAJIBU YA RUFAA YA AZAM FC YA KUPOKWA ALAMA 3

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.18,2016 SAA 01:39 USIKU

Timu ya Azam imepoteza rufaa yake ya kupinga kupokwa pointi tatu kwa kumchezesha Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za
njano.

Kamati ya saa 72 imethibitisha Nyoni alikuwa na kadi tatu za njano kabla ya mchezo dhidi ya Mbeya City, uliochezwa jijini Mbeya mwanzoni mwa msimu wa 2015-16.

Afisa habari wa TFF, Afred Lucas amesema kamati ya saa 72 imejiridhisha kwamba rufaa ya Azam FC haikua na mashiko kutokana na kanuni za ligi kuu kueleza wazi kwamba mchezaji akiwa na kadi tatu za njano hatoruhusiwa kucheza mchezo unaofuata.

Wakati TFF wakitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kuwekwa kapuni kwa rufaa ya Azam FC, mkuu wa idara ya habari ya klabu hiyo Jaffary Iddy amesema ni mapema mno kwao kuzungumzia jambo hilo ambalo halijawafikia kimaandishi.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .



Post a Comment

0 Comments