Ticker

6/recent/ticker-posts

DAAA! SIMBA SC KUSUBIRI TENA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.3,2016 SAA 02:11 USIKU

Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeahirisha michuano ya kuwania Kombe la nchi unakopita
Mto Nile ‘Nile Basin Cup’.
Taarifa iliyotumwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye inasema kwamba wamepata taarifa za kuahirisha michuano hiyo kutoka kwa waratibu wakiwamo wenyeji Sudan.
Taarifa imesema wamekubaliana kuahirisha mpaka hapo watakapotangaza tena hivyo basi,Simba iliyoteuliwa na TFF kushiriki michuano hiyo, imetaarifiwa kusubiri tarehe mpya ya mashindano.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .


Post a Comment

0 Comments