Pongezi kwa wachezaji wa klabu ya Young Africans, zimeendelea kumiminika kufuatia mafanikio waliyoyapata ya kutinga katika
hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho, pamoja na kutwaa ubingwa wa Tanzania bara msimu wa 2015-16.
hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho, pamoja na kutwaa ubingwa wa Tanzania bara msimu wa 2015-16.
Pongezi kwa wachezaji wa klabu hiyo kongwe kwa hii leo zimetolewa na baraza la wazee pamoja na viongozi wa matawi ya Young Africans, huku uongozi ulio chini ya mwenyekiti Yusuph Manji ukitajwa katika harakati za kupatikana kwa mafanikio hayo.
Katibu mkuu wa baraza la wazee wa Young Africans, Ibrahim Akilimali, amesema wamefikia hatua ya kutoa pongezi kwa wachezaji pamoja na uongozi baada ya kuona hakuna cha kuwapa zaidi ya kusema ahsante.
Hata hivyo baraza hilo la wazee limetoa wito kwa wanachama wote wa young Africans, kuwa macho katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, kutokana na chokochoko ambazo zinaweza kuanzishwa kwa makusudi.
Baraza hilo la wazee kupitia kwa katibu wao Ibrahim Akilimali, umesema unaamini kuna hila za makusudi zinazofanywa na baadhi ya watu, kwa lengo la kuibua migogoro katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.
Akilimali amesema kutokana na hila , wanayanga wenye mapenzi ya dhati hawatokubali kuona suala hilo likijitokeza.
SIKILIZA HAPA .
HHata hivyo Akilimali amewataka wadau wa soka nchini pamoja na watanzania kwa ujumla kutowaelewa vibaya, kutokana na kauli waliyoitoa kuhusu andiko lililowekwa kwenye gazeti moja la hii leo, linalomuhusu mwenyekiti wao Yusuph Manji.
Amesema wanatambua jambo hilo, lipo mahakamani na limeegemea katika masuala ya kibiashara ya mwenyekiti wao, lakini wanaamini huenda limefanywa kwa makusudi kutokana na wakati walionao kwa sasa kuhusu uchaguzi ulio mbele yao.

0 Comments