Ticker

6/recent/ticker-posts

RATIBA YA LIGI KUU TZ BARA WIKIENDI HII

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Apr.15,2016 SAA 07:41 MCHANA
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
Jumamosi, Young Africans watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Ndanda FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Nang’wanda Sijaona mjini Mtwara.

Coastal Union watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani jinini Tanga, huku Jumapili, Simba SC wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments